Ni habari kutoka kwa msanii Baba Levo ambaye amesema, wajumbe wameshamaliza kazi baada ya kushinda kura za maoni kwa asilimia 97 ili aweze kuwania Udiwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Baada ya kushinda kura za maoni Baba Levo ameeleza kuwa, atakayekuja kushindana naye bora aache kwani Kata ya Mwanga Kaskazini ni kata yake binafsi.

“Nashukuru chama changu cha ACT Wazalendo na Wajumbe kwa kunipa ridhaa na nafasi ya kuchukua fomu ya Udiwani, anayekuja kugombea Udiwani na mimi anatakiwa kujua kuna mwenyewe na Mwanga Kaskazini ni Kata yangu binafsi, waache kujisumbua na kupoteza pesa, tena bora hiyo pesa angeanzisha biashara hata ya vikoba kwa sababu kuniangusha haiwezekani” Baba Levo aliiambia EATV.

The post Baba Levo awashukuru wajumbe kura za maoni Udiwani Kata ya Mwanga Kigoma appeared first on Bongo5.com.