Bridger Walker, mtoto mwenye umri wa miaka 6, ameguka jasiri na kusifiwa na watu baada ya kumuokoa mdogo wake asishambuliwe na mbwa. Mbwa huyo aina ya Germany Shepherd alimkimbiza mdogo wake mwenye umri wa miaka 4, ndipo mtoto huyo alipokimbia na kumkinga mdogo wake asing'ate na mbwa huyo. Badala ya mbwa huyo kukimbia alimshambulia na kumchanachana shavuni. Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji uliochukua zaidi ya masaa mawili na kushona zaidi ya nyuzi 90 kwenye jeraha lake. Baba yake alisema baada ya kumuuliza kwanini aliamua kurukia kati ya mbwa na mdogo wake, Briger aliwajibu " niliona ikiwa mtu atakufa, basi ni lazima nife mimi na wala sio mdogo" ... story yao iko hapa @dr.paulmasua
#ngasatv