Mbunge wa Kinondoni aliyemaliza muda wake, Maulid Mtulia amesema kuwa yeye haoni sababu ya yeye kurudi chama cha CUF na kwamba ile picha iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ni ya siku nyingi.


Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa picha inayosambaa mitandaoni ni ya mwaka 2015,  hata yule anayeonekana pembeni yake alishafariki siku nyingi.

"Kwanini sasa nirudi CUF, siyo kweli mimi nipo tu, ile picha ni ya mwaka 2015 yule aliyekuwa pembeni anaitwa Rashid amefariki mwaka juzi, alikuwa anakaa Mzimu" amesema Mtulia.

Hivi karibuni ilisambaa picha ya Mtulia ikionesha kwamba amerudi chama chake cha zamani cha CUF