Kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, msanii wa BongoFleva Alikiba ameghairisha tamasha lake la Kigoma “Behewa la Ukarimu” ambalo alipanga kufanya siku ya Julai 31 mkoani humo.

Msanii wa BongoFleva Alikiba

Akitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram msanii Alikiba ameeleza kuwa  “Habari ndugu zangu Watanzania, kama wengi mlivyosikia Taifa letu limepata msiba wa baba na mlezi Mzee Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, ni msiba ambao nimeupokea kwa masikitiko imenifikia ghafla sana, lakini ni mapenzi ya Mungu naomba Mungu ampumzishe mahali pema

Kutokana na msiba huu mzito nimeahirisha show yetu ya Kigoma iliyokuwa ifanyike Julai 31 ili kushiriki  msiba huu wa kitaifa mpaka Agosti 14, pia nimehairisha zoezi la upokeaji michango mbalimbali ambalo nilipanga kulifanya kesho, taarifa za siku ya kupokea michango kwa ajili ya kuweka kwenye  Behewa la Ukarimu  nitatangaza baada ya msiba kumalizika ahsanteni, natoa pole kwa watanzania na wapambanaji wote walioguswa na msiba huu” ameongeza

Kupitia post zake za nyuma alitangaza kurudi nyumbani kwao kufanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza mkoani Kigoma baada ya kupita miaka 6.

View this post on Instagram

#Repost @officialalikiba with @make_repost ・・・ Habari ndugu zangu Watanzania, kama wengi mlivyosikia, taifa letu tumepata msiba wa Baba na Mlezi, Mzee Benjamin Mkapa aliekuwa rais wa awamu ya tatu, ni msiba ambao nimeupokea kwa masikitiko, imenifikia ghafla sana, lakini ni mapenzi ya Mungu. Naomba Mungu ampumzishe mahali pema Kutokana na msiba huu mzito nimeahirisha show yetu ya KIGOMA iliyokuwa ifanyike tarehe 31 ili kushiriki katika msiba huu wa kitaifa mpaka tarehe 14 August 2020. Pia nimehairisha zoezi la upokeaji wa michango mbalimbali ambalo nilipanga kulifanya kesho katika ofisi za Clouds Media Mikocheni. Taarifa za siku ya kupokea michango kwa ajili ya kuweka kwenye #BehewaLaUkarimu – nitatangaza baada ya msiba kumalizika. Asanteni, natoa pole kwa watanzania na wapambanaji wote walioguswa na msiba huu #KingKiba

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Alikiba aahirisha show yake ya Kigoma kutokana na msiba, Nimeahirisha na upokeaji wa michango yote appeared first on Bongo5.com.