Mabilionea Elon Musk, Jeff Bezos na Bill Gates ni miongoni mwa watu mashuhuri nchini Marekani ambao akaunti zao za mtandao wa twitter zilidukuliwa katika kashfa inayohusisha fedha za kidigitali mtandaoni Bitcoin.

Akaunti ya twitter ya aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, Joe Biden na Kanye West pia ziliombwa mchango wa fedha kwenye mfumo huo wa fedha za kidigitali.

”Kila mtu ananiambia nirudishe kwa jamii,” Ukurasa wa twitter wa Bwana Gates ulieleza. ”Tuma dola 1,000, nitakurudishia dola 2,000.”

”Siku ngumu kwetu Twitter. Tunasikitika kwa kilichotokea,” aliandika mwanzilishi wa mtandao huo Jack Dorsey siku ya Jumatano.

”Tunafanya uchunguzi na tutatoa taarifa kuhusu kila kitu tunachoweza tutakapojua hasa kilichotokea,” alieleza bwana Dorsey.

Awali, Twitter ilichukua hatua zaidi kwa kuzisitisha akaunti nyingi zilizoidhinishwa kwa alama ya buluu kufanya kazi .

Hali kadhalika maombi ya kubadilisha neno la siri yalikuwa yakikataliwa na ” na matumizi ya akaunti hiyo ” yalisitishwa.

Siku ya Alhamisi akaunti za watumiaji zilizoidhinishwa zilianza kufanya kazi tena, lakini Twitter ilisema kuwa ilikuwa bado inafanyia kazi.

Dmitri Alperoitch, mwanzilishi wa kampuni ya usalama mtandaoni ya CrowdStrike, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa : Hili ni tukio baya kuwahi kutokea kwenye mtandao huu mkubwa wa kijamii.

Katika akaunti ya Bwana Musk, Mkuu wa Tesla na SpaceX alitoa ahadi ya kutoa mara mbili ya malipo yoyote ya fedha za kigitiali kwenda kwenye akaunti yake ya fedha za mtandaoni ”katika kipindi cha dakika 30 zijazo”.

”Ninajisikia kujitolea kwa sababu ya Covid-19,” ukurasa wake wa twitter ulieleza, sambamba na anuani ya sarafu ya kidigitali.

Ujumbe wa twitter ulifutwa dakika chache tu baada ya kuchapishwa.

A hacked tweet from Elon Musk's account
Maelezo ya picha,One of the hacked tweets from Elon Musk’s account
Presentational white space

Na hayo yakiendelea akaunti ya twitter ya Elon Musk iliondolewa nyengine ikajitokeza , baadaye akaunti ya tatu ikajitokeza .

Mbali na mwanamuziki Kanye West, mkewe Kim Kardashian, aliyekuwa rais wa Marekani Obama, mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democrat Joe Biden, na mfanyabiashara wa chombo cha habari billionea Mike Bloomberg, makampuni makubwa ikiwemo Uber na Apple yalilengwa.

Kampeni ya Biden ilisema kwamba twitter ilifunga akaunti hizo katika kipindi cha dakika chache na kuondoa ujumbe uliochapishwa kuhusiana na kashfa hiyo.

Msemaji wa Bill Gates aliambia chombo cha habari cha AP kwamba hii inaonekana kuwa miongoni mwa masuala makubwa ambayo Twitter inakabiliana nayo.

BBC inaweza kuripoti kutoka chanzo cha usalama kwamba tovuti kwa jina cryptohealth.com ilisajiliwa na mshambuliaji wa mtandao alietumia anwani ya barua mkworth5@gmail.com.

Jina hilo “Anthony Elias” lilitumika kusajili tovuti hiyo.

Cryptohealth pia ilisajili akaunti ya instagram.

Ujumbe ulioandikwa ulisema ”Ilikuwa sisi” ukiwa na emoji ya uso unaotabasamu.

Wasifu wake wa Instagram pia ulichapisha ujumbe uliosema : lilikuwa shambulio la hisani, fedha zenu zitaelekea mahala pazuri.

Chapisho la instagram katika akaunti ya Cryptoforhealth

The post Akaunti za twitter za Obama, Jeff Bezos, Elon Musk, Joe Biden na Kanye West zadukuliwa katika kashfa ya Bitcoin appeared first on Bongo5.com.