Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewashukuru wana Kigamboni mapenzi yao makubwa waliyo yaonesha kwake.
Makonda ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku akisema kuwa amepata pole nyingi sana kutokana na matokeo ya hapo jana.
Nimepata pole nyingi sana kutokana na Matokeo ya jana.Kwanza nawashukuru kwa upendo wenu na Maombi yenu ya kunitakia mafanikio ktk kutimiza NDOTO yangu. Jambo moja Kubwa na Muhimu ni kuyajua Mapenzi ya Mungu na ktk hili Mapenzi ya Mungu ni Makubwa kuliko Mapenzi yangu. Nawatakia baraka na afya njema siku zote za Maisha yenu. Asanteni sana sana Wana KIGAMBONI kwa upendo wenu na kunipa nafasi niwe sehemu ya Maisha yenu.
Makonda alishindwa kwenye kura hizo za maoni na Faustine Engelbert Ndugulile aliyepata kura 190, huku yeye akifanikiwa kushika nafasi ya pili akiwa na kura 122.
The post Ahsante sana Wana Kigamboni – Paul Makonda appeared first on Bongo5.com.