Mtangazaji maarufu wa vipindi vya burudani mchana, Adam Mchomvu kutokea Clouds FM anatarajiwa kuonekana na kusikika leo Wasafi TV.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye kurasa za mitandano ya kijamii ya Wasafi TV ni kwamba Mchomvu ataonekeana saa tatu usiku.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza iwapo Mtangazaji huyo wa Show ya XXL kajiunga rasmi na Wasafi Media.

Ikumbukwe kuwa, takribani miezi miwili iliyopita, Mtangazaji mwingine wa aliyekuwa wa show hiyo, B Dozen alijiunga na E FM Radio/TV E Tanzania