Serikal ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya virusi vya Corona kupungua.
Taarifa hiyo imetolewa hivi punde na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmood Thabit Kombo ambapo amesema serikali imefikia uwamuzi huo baada ya kujiridhisha na kiasi kidogo cha maambukizi ya corona.
Waziri Kombo ameeleza pamoja na serikali kuruhusu shughuli za utalii kuendelea ni vyema shughuli hizo zikaendeshwa kwa kuzingatia tahadhari ya virusi vya corona kwa wageni kupimwa kila wanapoingia nchini, na wageni wote kutakiwa kuwa na bima zao za afya kabla hawajingia nchini.
The post Zanzibar waruhusu ndege za kitalii kuanza kutua appeared first on Bongo5.com.