Msanii wa muziki @youngdaresalama amejipanga kuachia documentary ambayo itaonesha jinsi alivyoachana na matumizi ya Dawa za Kulevya.


Rapa huyo amesema “Speaking of Madawa ya Kulevya! Kuna muda nikikumbuka baadhi ya mapito yangu huwa naishia kucheka tu. Mwaka 2016 nilipambana sana kuachana na hili swala, kwa msaada wa watu wengi. Haikuwa rahisi washkaji zangu, ila Mungu yu nami na alinipigania sana.
Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kunisaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya (Hivi karibuni Documentary yangu ikitoka, mtajua namna nilivyoingia kwenye hilo swala). Sababu ya kwanza ilikuwa ni team yangu ya kipindi kile ya MDB. Kusema ukweli hawa watu walipambana sana na jambo langu, nadhani sikupigwa makofi tu 😀 ila niliwakwaza sana. Walipambana sana kunitoa huko. Japo haikuwa rahisi hata kidogo,

Sababu ya Pili ni Mh. @baba_keagan na kampeni ya kuzuia madawa. Ile ilikuwa na matokeo chanya sana kwa jamii hasa kwangu mimi. Najua Mh. Makonda alipigwa vita sana kwenye swala lile, na najua wapo ambao hadi leo wanaliona jambo lile lilikaa kisiasa, lakini mimi nina ushuhuda wa namna kampeni ile ilivyonisaidia mimi binafsi, na baadhi ya vijana ninaowafahamu, ambao leo hii tunaendesha maisha yetu na familia zetu baada ya kulazimika kuacha kabisa matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na shinikizo la serikali.
Wazee, msichokijua ni kwamba kuna siku nilizidisha dozi, nikajiona kabisa nakufa. Siku hiyo nilisali sala mbili, ya kwanza ni ya mwisho, na ya pili ilikuwa ya kumuomba Mungu anivushe ule usiku tu, nami nilimuahidi kuto kurudia tena na shughuli hizo. (Story nyingi mtazipata kwenye Documentary yangu); @baba_keagan kwa namna moja au nyingine najua ulikutana na changamoto kubwa sana wkt wa kampeni ile, kwasababu ulipigana vita kubwa sana. Mimi na familia yangu tuchukue fursa hii kwanza kukupa pole kwa kadhia zote ulizokutana nazo, na pia naomba niseme asante sana kwa kuileta. Imenisaidia sana, huenda leo hii ningekuwa teja kabisa nisiye na thamani machoni mwa watu, lakini kwa Nguvu za Mungu, leo naweza kuandika hapa na kushare a positive note kutoka kwenye janga negative kwenye maisha yetu vijana.,”