Klabu ya Yanga imempiga faini ya shilingi Mil 1,500,000 mchezaji Bernard Morrison kwa kosa la kuongea na vyombo vya habari kambini, bila kufuata kanuni za klabu, jambo ambalo ni kuhujumu na kukiuka taratibu na kanuni za klabu huku akiwa na nia ovu.

Mbali na hilo Yamga wameeleza kuwa Morrison ana mkataba wa miaka miwili ambapo waliongeza mkataba huo baada ya kuridhishwa na kiwango cha mchezaji, Mkataba ambao unamalizika mwaka 2022, lakini mchezaji katika mahojiano hayo alisema kuna vitu vingi mashabiki hawavijui na mkataba wake unamalizika mwezi ujao ambao ni julai.

The post Yanga yampiga faini ya mil 1.5 Morrison, waeleza sababu hizi appeared first on Bongo5.com.