YANGA, leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga leo Juni 13.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Yanga ilianza kwa kasi kushambulia lango la Mwadui FC na kupata bao la kuongoza dakika ya sita.Mapinduzi Balama aliifungia Yanga bao hilo dakika yasita akimaliza pasi ya Deus Kaseke.

Ushindi huo unaifanya Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael kubeba pointi zote tatu muhimu na kusepa nazo.

Inafikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 28 ikiwa sawa na Azam FC yenye pointi 54 ila wametofautiana kwenye mabao ya kufunga.

Yanga imefunga mabao 32 huku Azam FC ikiwa na mabao 37.