LEO Juni 13 Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael itakuwa na kibarua cha kumenyana na Mwadui FC.

Itaingia uwanjani bila kuwa na huduma ya wachezaji wake 7 ambao ni :-Ally Mtoni ‘Sonso’,Andrew Vincent ‘Dante’ na Rafael Daud ambao wanaumwa. All Ally na Eric Kabamba wameachwa kwa sababu ni mpango wa mwalimu kuwatumia wakati ujao.

Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha bado hajawa sawa kiafya huku nyota mwingine Bernard Morrison naye akiwa yupo Bongo.

Habari zinaeleza kuwa Morrison aligoma kujiunga na timu Shinyanga na nafasi yake ilichukuliwa na David Molinga.