Hali bado inaweza kuwa mbaya zaidi wakati huu wa janga la Covid-19, Shirika la afya duniani (who) limetahadharisha, miezi sita ikiwa imepita tangu mlipuko wa ugonjwa huo kutokea.

Mkuu wa shirika hilo, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema virusi vinaweza kuathiri watu wengi zaidi ikiwa serikali hazikuanza kutekeleza sera sahihi.

Ujumbe wake ulibaki kuwa ”Pima, fuatilia, tenga na weka karantini”, alisema.

Zaidi ya watu milioni 10 wamethibitishwa kuwa na maambukizi duniani tangu virusi hivyo vilipojitokeza nchini China mwishoni mwa mwaka jana.

Idadi ya wagonjwa waliopoteza maisha sasa ni zaidi ya 500,000

Nusu ya idadi ya watu walioambukizwa duniani imekuwa Marekanni na Ulaya, lakini idadi inaongezeka kwa kasi Amerika.

Virusi hivyo pia vinaathiri Kusini mwa Asia na Afrika, ambako hakutarajiwi ongezeko la juu mpaka mwishoni mwa mwezi Julai.

Dkt Tedros akitoa hotuba yake siku ya Jumatatu alisema: ”Sote tunataka hali hii kuisha. Sote tunataka kuendelea na maisha yetu. Lakini ukweli ulio mchungu ni kuwa bado hali hii haijafikia kuisha hata kidodo”

” ingawa nchi nyingi zimepiga hatua, bado ugonjwa huu unashika kasi duniani.”

”Kukiwa na wagonjwa milioni 10 sasa na vifo vya watu nusu milioni, mpaka pale matatizo yaliyogundulika yatakajulikana na WHO, ukosefu wa umoja wa kitaifa na kidunia na dunia iliyogawanyika hali inayosaidia kusambaa kwa virusi…bado hali itakuja kuwa mbaya zaidi,” alisema.

”Samahani kwa kusema hivyo, lakini kwa mazingira ya namna na hali hii, tunahofu hali kuwa mbaya .”

Amezitaka serikali kufuata mifano ya Ujerumani, Korea Kusini na Japan, ambazo zimekuwa zikichukua hatua kudhibiti maambukizi kwa kutumia sera ikiwemo vipimo na ufuatiliaji.

A person being tested for Covid-19
Maelezo ya picha,Kupima ni hatua ya kwanza ya kudhibiti janga la ugonjwa

Nchi gani zimeathirika zaidi?

Marekani imeripoti kuwa na watu milioni 2.5 walioathirika na vifo karibu 126,000 vilivyotokana na Covid-19 mpaka sasa- zaidi ya taifa jingine lolote.

Majimbo ya nchini Marekani katika wiki za hivi karibuni- hasa kusini yameripoti ongezeko la maambukizi mapya.

Ongezeko hilo limefanya maafisa wa Texas, Florida na majimbo mengine kuweka mazuio makali tena kwenye biashara.

Nchi ya pili iliyo na kiasi kikubwa cha maambukizi ni Brazil, iiwa na watu walioambukizwa milioni 1.3 na vifo zaidi ya watu 57,000.

Siku ya Jumatatu hali ya dharura ilitangazwa katika mji mkuu Brisilia, kutokana na ongezeko la maambukizi.

Kama ilivyo kwa magavana wengi wa Brazil na meya, mamlaka za serikali za maeneo, mjini Brasilia masharti ya kutochangamana yalipunguzwa makali mwanzoni mwa mwezi huu na kuruhusu kufunguliwa kwa maduka, nchini Uingereza – nchi yenye idadi kubwa ya vifo eneo la Magharibi mwa Ulaya- Meya wa Leicester alisema vilabu vya pombe na migahawa vinaweza kuendelea kufungwa kwa wiki mbili zaidi kutokana na ongezeko la watu walioambukizwa.

Passengers wait for a bus in Colombo, Sri Lanka

The post WHO yatahadharisha kuhusu Corona, hali kuwa mbaya siku za usoni appeared first on Bongo5.com.