Kanisa moja kutoka korea kusini linaloitwa Shincheonji church of Jesus lilisema Zaidi ya waumini wake 4,000 wameweza kupona corona(covid19) na wako tayari kujitolea utegili kwa ajili ya uvumbuzi wa matibabu mapya.

Kiasi cha damu kitachotolewa na waumini hao 4,000 kitakuwa na thamani ya trilioni 192 na bilioni 394 kwa kila mmoja kujitolea 500ml, Kutokana na tafsiri ya marekani “ni ngumu kupatikana kwa dawa dhidi ya corona kwa uharaka kutokana na utayari hafifu wa wagonjwa waliopona kujitolea damu zao ambapo ni 200 tu waliokuwa na utayari wa kujitolea. Kiwango hiki kikubwa cha msaada kutoka kwa wagonjwa hawa waliopona kutoka kanisa la Shincheonji church of Jesus litaleta utatuzi wa ukosefu wa damu kwa ajili ya utafiti” aliyaongea afisa mmoja kutoka Green cross pharma,kampuni ya biopharmaceutical kutoka korea kusini.

Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, ugonjwa huu unaoenea kwa kasi uliwakumba waumini wa kanisa la Shincheonji Church of Jesus katika mji wa daegu nchini korea kusini, ambapo dalili za mwanzo za janga hili lililotokana na utata katika ujio mkubwa wa wageni kutoka China kabla ya maambukizi kuwakumba waumini wa kanisa hilo.

Mr Man Hee Lee mwanzilishi wa kanisa hili la Shincheonji Church of Jesus alisema waumini wa kanisa hilo wameombwa kujitolea utegili(plasma) kwa hiali yao wenyewe “kama Yesu alivyojitoa sadaka kwa damu yake kwa ajili ya uhai, na tumaini letu ni kwamba damu hizi za watu waliojitolea zitaleta matokeo chanya katika kulishinda janga hili” alisema Mr Lee.

“Tulikuwa na majadiliano na maafisa wa afya ilikutengeneza mpango madhubuti kwa undani Zaidi, kwa ajili ya utoaji wa msaada wa damu , baadhi ya waumini waliopona wameshaanza kujitolea, tunashukuru kwa usaidizi wa serikali na timu za matibabu, kwani wameonesha utayari wao wa kujitolea kwa jamii” Alisema afisa wa kanisa.

Baadhi ya serikali za mitaa nchini korea kusini hivi karibuni wameleta mashtaka dhidi ya kanisa kwa madai kwamba kanisa halikutoa ushirikiano kwa mamlaka kwa kutowasilisha orodha yote ya vifaa vyote vya kanisa na waumini.

“hakuna ushahidi ulioletwa kwamba Shincheonji ilitoa orodha ambayo imebadilisha au haijakamilika na kulikuwa na utofauti mdogo tu ” alisema Kim kang-lip makamu waziri wa afya, utafiti wa kitaalamu kwa Shincheonji na covid19 ulisema kwamba kanisa lilitoa orodha kwa wanachama wa korea kusini, siku sita baada ya ombi ya orodha hiyo, “na ilikuwa haijafafanuliwa kwamba vifaa na mali ambazo zilisimamishwa zilitakiwa ziwekwe kwenye orodha”
, pale ambapo serikali ilipomba orodha ya mali zisizohamishwa.

(Shincheonji na virusi vya corona nchini korea kusini: upangaji wa kweli na uongo(hadithi)-karatasi nyeupe
https://bit.ly/3fZazyG)
Afisa habari wa Shincheonji alisema kanisa litashirikiana kwa ukamilifu na mawakala za serikali katika uchunguzi.

Korea kusini imeripoti kesi 12,535 na vifo 281 vilivyotokana na corona(covid19)

The post Waumini 4,000 waliopona corona korea kusini wajitolea utegili yenye thamani ya trilioni 192 na bilioni 394 za kitanzania kwa ajili ya tiba ya coronaYeah appeared first on Bongo5.com.