Wafanyakazi wanne wa Ikulu ya rais nchini Kenya wamepatikana na virus vya Corona.Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu Kanze Dena, wafanyakazi hao waligunduliwa wameambukizwa COVID-19 baada ya kufanyiwa uchunguzi Alhamisi, Juni 11.

State House (Kenya) - Wikipedia

Maafisa hao walioambukizwa wamelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wanaendelea kupata matibabu .

Msemaji wa Ikulu amewahakikishia Wakenya kuwa Rais Kenyata na familia yake wake wako salama na wamethibika kutokuwa na maambukizi ya corona.

”Ikulu inawafahamisha Wakenya kwamba rais na familia yake hawana ugonjwa wa Covid-19”, ilisema taarifa ya Bi Kanze Dena.

Taarifa hiyo pia iliwakumbusha Wakenya kwamba kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.

Katika juhudi za kuzuia maambukizi ya Corona, wafanyakazi wote wanaoishi nje ya Ikulu pamoja na wageni wamedhibitiwa kwa kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara ya Afya.

Kufikia sasa Kenya ina jumla ya watu 3,727, walioambukizwa virusi vya corona kufuatia ongezeko la wagonjwa wengine wapya 133.

Katika taarifa za kila siku kuhusu muenendo wa ugonjwa wa corona nchini Kenya, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema kuwa wagonjwa 33 waliokuwa wamelazwa hospitali wameruhusiwa kuenda nyumbani katika kipindi cha saa 24 na kufikisha 1,286 jumla ya watu waliopona ugonjwa wa corona.

Juni 6, Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kuongeza marufuku ya kutotoka nje nchini Kenya, shughuli za usafiri katika kaunti ya Nairobi na Mombasa zimesitishwa kwa siku 30 zaidi.

Bwana Kenyatta aliondoa marufuku ya kutotoka nje katika maeneo ya Eastleig, na Old Town kuanzia saa kumi asubuhi tarehe 7, Juni, 2020.

Kaunti za kwale na Kilifi pia zilifunguliwa kuanzia saa kumi asubihi 7, Juni 2020 kwa sababu maambukizi yameanza kupungua katika maeneo hayo.

Wakati huohuo, rais alilegeza masharti ya kutotoka nje usiku ,hatua ya kusalia ndani sasa itaanza kuwanzia saa tatu usiku hadi kumi asubuhi.

Bwana Kenyatta alifafanua kuwa kama kulegeza masharti kwa asilimia 20 kungesababisha maambukizi laki 2 na vifo 30,000 kufikia Desemba.

” Ikiwa masharti yangelegezwa kwa asilimia 60, kilele chake kingefikia Oktoba na maambukizi 450,000 na vifo 45,000,” rais amesema.

Rais alitoa mifano ya nchi zingine kama Korea Kusini, Pakistan na Malaysia na kuweka bayana kwamba ukosefu wa mchakato makhususi wa kufungua tena shughuli maambukizi yanaweza kuongezeka zaidi au kupata wimbi la pili la maambukizi.

Kwa mifano ya Kenya, kituo kilichotengwa cha Siaya kina vitanda kumi na tayari watu 9 wamelazwa ambapo kituo cha Busia kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa Covid-19 kina vitanda 34 na kituo hicho kilijaa wagonjwa siku mbili zilizopita.

Tangazo lingine lilikuwa shule kufunguliwa kuanzia Mosi, Septemba.

Baada ya kushauriana na washika dau wa elimu, rais amesema wizara ya elimu pamoja na ya afya, itatangaza mwongozo mpya wa elimu na kuonesha vile hali ya kawaida katika taasisi za masomo itakavyorejelelewa taratibu kuanzia muhula wa tatu kuanzia Septemba mosi, 2020. Wizara ya elimu pia itatarajiwa kutangaza kalenda mpya ya shule katikati ya Agosti.

The post Wanne wakutwa na Virusi vya Corona kutoka ndani ya Ikulu ya Kenya appeared first on Bongo5.com.