Jeshi nchini Mali, linasema maafisa wake wameauwa na wengine hawajuliakani walipo baada ya kushambuliwa na wanajihadi, katikati ya nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo zaidi ya 60 walikuwa kwenye msafara wakati waliposhambuliwa katika eneo la Bouka Were, umbali wa Kilomita 100 kutoka katika mpaka wa Mauritania.

Baada ya tukio hilo, ripoti za kijeshi zinaeleza kuwa ni wanajeshi 20 ndio waliopatikana, ikiwa na maana kuwa idadi ya waliouawa au kutoweka ni 40 huku msako wa kuwatafuta ukiendelea.

Hili ndilo shambulizi la hivi punde dhdii ya wanajeshi wa M ali; lkatika taifa hilo ambalo limeendelea kushuhudia ukosefu wa usalama tangu mwaka 2012 karibu na mipaka ya Burkina Faso na Niger.

Maelfu ya raia wamepoteza maisha kutokana na utkosefu wa usalama licha ya kuwepo kwa maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na wale wa Umoja wa Mataifa MINUSMA.

-RFI