Jumla ya wanajeshi 20 wa India wameuawa wakati wa makabiliano ya mpakani, kati yao na vikosi vya China. Jeshi la India limesema hayo jana, baada ya wiki kadhaa za machafuko.

India-China Border Clash Updates: 20 Indian soldiers killed in ...

Kwenye taarifa, jeshi la India limesema makabiliano yalizuka usiku wa kuamkia jana, katika bonde la Galwan wakati wa kutuliza machafuko.

Hii ni mara ya kwanza katika miongo mingi kwa mataifa hayo mawili makubwa barani Asia kukabiliana. Awali, jeshi la India liliripoti vifo vya wanajeshi watatu, lakini idadi hiyo imeongezeka baada ya wengine 17 waliojeruhiwa kufariki.

Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya China imethibitisha makabiliano hayo, lakini bila ya kutoa maelezo kuhusu vifo. Lakini gazeti la Global Times linalodhibitiwa na serikali ya China, limeripoti kwamba vifo pia vilitokea miongoni mwa wanajeshi wa China. China imeituhumu India kwa kuvuka mpaka wa eneo linalozozaniwa kati ya nchi hizo mbili.

The post Wanajeshi 20 wa India wauawa na vikosi vya China appeared first on Bongo5.com.