Kenya imerekodi idadi kubwa ya maambukizi mapya katika muda wa saa 24 baada ya maambukizi mapya 184 kuthibitishwa na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 4044.

Naibu Waziri wa Afya Rashid Aman amesema kuwa watu hao wamethibitishwa baada ya sampuli  2518 kuchunguzwa.

Idadi ya waliopona imefikia 1,354 baada ya wagonjwa 27 kupona na kuondoka hospitalini.

Hata hivyo idadi ya vifo imefikia 107 baada ya watu wawili zaidi kuaga dunia.