Mwanamke mmoja na mpwa wake wamefikishwa Mahakamani nchini Uganda wakituhumiwa kuingia nyumbani kwa Mwanaume na kujificha juu ya dari kisha kumrekodi video wakati akijamiiana na baadaye wakamtaka alipe Mil 1.5 ya Uganda (zaidi ya Tsh.Laki 9), ili wasivujishe video hiyo.