Shirika la Afya Duniani (WHO) limefurahishwa na matokeo ya awali ya majaribio ya dawa ya kutibu corona Uingereza yanayoonesha kwamba dawa ya dexamethasone, inaweza kuokoa maisha ya watu walio mahututi wanaougua ugonjwa wa Covid-19.

Kwa wagonjwa wanaotumia mashine za kupumua, dawa hiyo ilionesha kwamba imepunguza idadi ya vifo kwa theluthi moja, na kwa wagonjwa wanaohitaji hewa ya oksijeni, idadi ya vifo ilipungua kwa humusi au moja ya tano kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa na WHO.

Hata hivyo, faida ama uzuri wa dawa hiyo kulijitokeza kwa wagonjwa wanaoumwa sana kwasababu ya virusi vya corona wala sio kwa wenye athari za wastani za ugonjwa huo.

“Hii ndio dawa ya kwanza kupunguza idadi ya vifo kwa wagonjwa wa virusi vya corona wanaohitaji oksijeni au walio kwenye mashine za kupumua,” amesema Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

“Hii ni habari njema na ninapongeza serikali ya Uingereza, Chuo Kikuu cha Oxford, na hospitali nyingi na wagonjwa Uingereza ambao wamechangia katika utafiti huu wa kisayansi ambao ni mwokozi wa maisha.”

Dexamethasone inaweza kusaidia maisha ya wagonjwa wa virusi vya corona waliopo katika hali mahututi.Dexamethasone inaweza kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wa virusi vya corona waliopo katika hali mahututi.

Dexamethasone ni dawa ambayo imekuwa ikitumiwa tangu 1960 kupunguza uvimbe katika hali tofauti kama vile ugonjwa wa saratani, yabisi kavu na kadhalika.

Watafiti walishirikishana maoni yao ya awali kuhusu matokeo ya majaribio ya dawa hiyo na WHO, huku wakitarajia utafiti wa kina wa data siku za hivi karibuni.

Dawa ya bei rahisi inayopatikana kwa urahisi Dexamethasone inaweza kusaidia maisha ya wagonjwa wa virusi vya corona waliopo katika hali mahututi.

Wataalam wa Uingereza wanasema kwamba tiba hiyo yenye steroid ni hatua kubwa iliopigwa katika kukabiliana na virusi hivyo hatari.

Inapunguza hatari ya mtu kufariki kwa thuluthi moja miongoni mwa wagonjwa walio katika mashine za kuwasaidia kupumua.

Kwa wale wanaotumia oksijeni inapunguza hatari ya kifo kwa kiwango kikubwa.

Dawa hiyo ni miongoni mwa majaribio ya tiba ya corona duniani kuona iwapo inaweza kusaidia kutibu corona.

Watafiti wanakadiria kwamba iwapo dawa hiyo ingekuwepo nchini Uingereza kuanzia mwanzo wa mlipuko wa corona , hadi maisha ya watu 5000 yangekuwa yameokolewa.

Kwasababu ni ya bei rahisi inaweza kuyasaidia pakubwa mataifa masikini yanayotatizika katika kukabliana na ugonjwa wa Covid-19.

Inaokoa maisha

wagonjwa wafanyiwa vipimo

Wagonjwa 19 kati ya 20 wanaopata virusi vya corona hupata nafuu bila kwenda hospitalini .

Kati ya wale waliolazwa hospitalini , wengi wao hupata nafuu , lakini wengine wangehitaji oksijeni ama mashine za kuwasaidia kupumua .

Hawa ni wagonjwa ambao wapo katika hali mahututi na wanasaidiwa na dexamethasone.

Dawa hiyo tayari inatumika kupunguza uvimbe katika magonjwa tofauti, na inaonekana inaweza kuzuia uharibifu ambao unaweza kufanyika wakati kinga ya mwili inapungua wakati inapokabilana na hirusi vya corona.

Hatua ya mwili kuongeza juhudi zake za kukabiliana na virusi hivyo inaweza kuwa ya kufa na kupona.

Katika majaribio hayo yalioongozwa na Chuo kikuu cha Oxford , takriban wagonjwa 2000 wa hospitali walipatiwa dexamethasone na walililangishwa na wengine 4000 ambao hawakupatiwa tiba hiyo.

Kwa wagonjwa waliokuwa katika mashine za kuwasaidia kupumua ilipunguza hatari ya kufariki kutoka asilimia 40 hadi 28 . Kwa wagonja waliohitaji Oksijeni ilipunguza hatari ya kifo kutoka asilimia 25 hadi 20.

Hospital bed

Mchunguzi mkuu Profesa Peter Horby alisema: Hii ndio dawa pekee kufikia sasa ambayo imeonesha kupunguza hatari ya kifo na inapunguza kwa kiwango kikuu., ”ni mafanilkio makubwa”.

Mtafiti aliyeongoza uchunguzi huo Profesa Martin landray anasema kwamba ugunduzi huo una maana kwamba kati ya wagonjwa wanane wanaohitaji mashine za kusaidia kupumua unaweza kuokoa maisha ya mtu mmoja.

Miongoni mwa wagonjwa wanohitaji Oksijeni , unaokoa maisha ya mtu mmoja kati ya wagonjwa 20-25 waliotibiwa na dawa hiyo.Kuna faida ilio wazi .

Tiba hiyo inatumika kwa siku 10 na inagharimu dola tano kwa mgonjwa. Hivyobasi inagharimu dola 35 kuokoa maisha. Hii ni dawa ambayo inapatikana kote duniani.

Profesa landray alisema Hospitali zinapaswa kuitumia bila kuchelewa lakini watu hawafai kuinunua ili kupeleka nyumbani.

Dawa hiyo hatahivyo haionekani kuwasaidia wagonjwa wenye dalili chache- watu wasiohitaji usaidizi wa kupumua.

Majaribio hayo ya kuokoa maisha yamekuwa yakifanyika tangu mwezi Machi na yalihusisha dawa ya malaria hydroxychloroquine ambayo imeondolewa katika majaribio hayo kutokana na wasiwasi kwamba inaongeza vifo miongoni mwa wagonjwa walio na matatizo ya moyo.

Dawa nyingine kwa jina remdesvir , dawa inayotibu virusi inayoonekana kupunguza muda wa mtu kupona corona tayari imekuwa ikitumika na Idara ya Afya nchini Uingereza NHS.

corona

Uchanganuzi wa Fergus Walsh – mwandishi wa maswala ya Afya.

Dawa ya kwanza iliothibitishwa kupunguza vifo vinavyotokana na Covid-19 sio mpya na ghali bali ni dawa ya zamani ilio bei rahisi.

Hili ni suala la kupongezwa kwasababu inamaana kwamba wagonjwa wote kote duniani watafaidika mara moja.

Matokoe ya vipimo hivyo yametolewa kwa haraka kwasababu athari zake zitakuwa kubwa duniani.

Dexamethasone imekuwa ikitumika tangu miaka ya 60 kutibu magonjwa tofauti kama vile baridi yabisi na pumu. Nusu ya wagonjwa wote wa Covid wanaohitaji kipumuzi hufariki , hivyobasi dawa hiyo hupunguza hatari hiyo kwa thuluthi moja ni ufanisi mkubwa.

Dawa hiyo hutumika kupitia sindano katika chumba cha wagonjwa mahututi na kupitia tembe kwa wagonjwa wasio katika hali mahututi .

Dawa ya pekee iliothibitishwa kuwasaidia wagonjwa wa Covid-19 ni remdesvir, dawa ya virusi ambayo imekuwa ikitumiwa kutibu Ebola

Dawa hiyo imeonesha kuwa na uwezo wa kupunguza muda unaotumika kuonesha dalili za ugonjwa wa corona kutoka siku 15 hadi 11 , lakini ushahidi haukuwa na thibitisho la kuonesha kwamba unaweza kupunguza kifo.

Ikilinganishwa na dexamethasone, remdesivir ni dawa mpya ambayo haijasambaa kote duniani na bei yake haijatangazwa.

The post UINGEREZA: Hii ndio dawa ya Corona iliyobainika kutibu baada ya majaribio appeared first on Bongo5.com.