Wizara ya Afya imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 15 na visa vya COVID19 nchini humo vimefikia 522 huku idadi ya waliopona ikiwa 82.

Katika wagonjwa hao 15, wanne ni madereva wa malori waliotokea Tanzania, 2 ni madereva kutoka Busia na 9 ni watu waliokuwa karibu na wagonjwa ambao tayari wamethibitishwa na Mamlaka

Aidha, madereva wa malori 33 waliokutwa na #CoronaVirus wamezuiwa kuingia Uganda na kurudishwa nchini mwao

Wizara imeendelea kuwasisitiza wananchi kuvaa barakoa wanapokuwa maeneo ya umma, kunawa mikono na kuzingatia umbali wa mita mbili baina ya mtu na mtu

The post Uganda watangaza visa vipya 15 vya corona, 82 wapona appeared first on Bongo5.com.