Katika suala la virusi kuna tofauti ndogo kati ya uharibifu na usambazaji wake.Virusi hivyo vinaposambaa kwa kiwango cha juu humuua ama kumzuia mtu kuendelea na hali yake ya kawaida.

Kwa upande mwengine, iwapo vitafanya uharibifu mdogo havina uwezo wa kuzaana ili kuweza kusababisha maambukizi zaidi. Lakini Virusi vya SARS-CoV-2, vinavyosababisha Covid-19 ni tofauti na nadharia hii.

Dalili zake mara nyingi hazionekani hadi pale mtu aliyembukizwa anapokuwa akisambaza virusi hivyo kwa siku kadhaa.

Utafiti wa virusi vya Covid-19 ulikadiria kwamba kiwango kikuu cha maambukizi ya virusi hivyo hutokea siku moja au mbili kabla ya mtu aliyeambukizwa kuanza kuonyesha dalili.

Kwa ufupi , utajihisi mgonjwa wakati virusi hivyo vimeafikia lengo lake la kusambaa.

Virusi vina tabia ya kuzaana na kuingia katika mtu mwengine na husambaa hadi kinga ya mwili ya mtu aliyeambukizwa itakapofanikiwa kukabiliana navyo

Covid-19Utafiti wa hivi karibuni uliofanyiwa SARS-CoV-2 unaonesha kwamba kati ya asilimia 40 na 45 ya wale walioambukizwa huwa hawana dalili.

Uharibifu unaosababishwa na virusi huvizuia kusambaa zaidi. Hii ndio imekuwa tabia ya virusi vingine kama vile Marburg, Ebola na SARS.

Milipuko inayosababisha dalili kali ni rahisi kuikabili kupitia masharti ya kiafya kwasababu walioambukizwa ni rahisi kuwatambua.

SARS-CoV-2 hatahivyo vinaweza kushambulia jamii kwasababu watu wengi walioambukizwa hawaoneshi dalili zozote.

Kwanini vinafanana na magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono

Kutokana na uchambuizi huo, Covid-19 inafanana na ugonjwa uliosambazwa kupitia ngono.

Mtu alieambukizwa anaendelea kuishi bila dalili huku akiendelea kusambaza maambukizi kwa wengine.

Virusi vya ukimwi na ugonjwa wa kaswende kwa mfano ni magonjwa yasio na dalili kwa kipindi cha muda mrefu wa maambukizi.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanyiwa SARS-CoV-2 unaonesha kwamba kati ya asilimia 40 na 45 ya wale walioambukizwa huwa hawana dalili.

Na walioambukizwa wanaweza kusambaza virusi hivyo kwa muda mrefu.

Kuna ushahidi kwamba uwezo wa kukabiliana na maambukizi upo tofauti miongoni mwa waathiriwa.Kuna ushahidi kwamba uwezo wa kukabiliana na maambukizi upo tofauti miongoni mwa waathiriwa.

Covid-19 una tabia nyengine inayofanana na magonjwa mengi ya ngono.

Athari zake sio sawa kwa walioambukizwa na tofauti hizo zinashangaza.

Kuna ushahidi kwamba uwezo wa kukabiliana na maambukizi upo tofauti miongoni mwa waathiriwa.

HospitaliVirusi vya SARS-CoV-2 – ama vimelea vingine – havibadili sababu yao ya kutaka kutumia miili yetu kama chombo cha kuvisafirisha na kusababisha maambukizi zaidi

Virusi vya SARS-CoV-2 – ama vimelea vingine – havibadili sababu yao ya kutaka kutumia miili yetu kama chombo cha kuvisafirisha na kusababisha maambukizi zaidi , lakini vimelea vinaweza kubadilika kwa njia ambayo inaweza kuonekana kana kwamba vinafanya mchezo na miili yetu.

Utafiti unaonesha kwamba vimelea vinaweza kusambaa zaidi kwa mtu mmoja na kutofanya hivyo kwa mtu mwengine kutokana na hali ya mtu huyo kama vile umri, uwepo wa maambukizi mengine na kinga ya mtu.

Jinsi virusi vya corona vinavyopenya mwilini.

Umri, kufikia sasa unaonekana kuwa sababu muhimu.

Watu walio na umri mkubwa huathirika pakubwa na maambukizi, huku vijana wakiathirika kidogo licha ya kwamba huenda wameathiriwa kwa njia sawa.

Hii ni kwasababu watu tofauti wana kinga tofauti.

Sababu nyengine ni kwamba tunazidi kuzeeka , kuna uwezekano wa kuanza kupata magonjwa mengine kama vile kunenepa kupitia kiasi , shinikizo la damu mwilini, sababu inayoweza kusababisha uharibifu kutoka kwa SARS-CoV-2.

HospitalBaadhi ya tafiti zinasema kwamba watu wenye umri mdogo mara nyingi hukosa kuonesha dalili za virusi hivyo.

Baadhi ya tafiti zinasema kwamba watu wenye umri mdogo mara nyingi hukosa kuonesha dalili za virusi hivyo.

Hatahivyo walio na dalili na wasio na dalili wote wanaweza kusababisha maambukizi ya virusi hivyo.

The post Uchunguzi waonesha Corona haina tofauti na magonjwa ya ngono, Fahamu zaidi appeared first on Bongo5.com.