Wakati joto la uchaguzi likizidi kupamba moto hapa nchini nafasi ya ubunge jimbo la Arusha mjini ndani ya CCM imegeuka kaa la moto baada ya vigogo kadhaa kupigana vikumbo

Baadhi ya vigogo hao ni pamoja na Mfanyabiashara Maarufu mkoani Arusha Phillemon Mollel au MONABAN ,aliyekuwa meya wa Arusha,Kalist Lazaro ,Mrisho Gambo ambaye alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.

Wengine ni pamoja na Albert Msando wakili wa kujitegemea ,Lengai Ole Sabaya Mkuu wa wilaya ya Hai na Thomas Munis mfanyabiashara wa Madini jijini Arusha na wengine kibao.

Kalisti Lazaro ambaye anatajwa kuonyesha nia ya kugombea jimbo hilo kupitia ccm,amejipatia umaarufu mkubwa zaidi kutokana na uchapakazi wake akiwa Meya wa jiji la Arusha akitokea chadema ila anaweza asikubalike sana kwa wanaccm kwa sababu ya ugeni ndani ya chama hicho.

Kabla ya kuwa Meya wa Arusha,Lazaro alimaarufu BUSH aliwahi kuwa diwani ,Mwenyekiti wa kijiji na kiongozi shupavu katika vyama mbalimbali vya siasa alivyopitia kikiwemo CHADEMA ,CCM na TLP.

Kalisti anatajwa kama mwanasiasa asiye na makundi na mwenye kupenda kushirikiana na viongozi wa serikali na ndoto yake ni kupata ubunge ili aweze kuwatumikia wananchi kwa maendeleo.

Mfanyabiashara maarufu ,Philemon Mollel au MONABAN ambaye ameonyesha nia ya kusaka ubunge jimbo la Arusha Mjini,aliwahi kuwa kamanda wa Vijana wa UVCCM mkoa wa Arusha,Mgombea Ubunge mwaka 2015 (ccm)Mtumishi wa Mungu na mwanajamii anayependa kujitoa kusaidia makundi yenye uhitaji na mchango wake wa kuwavua udiwani madiwani wa chadema nankujiunga na ccm ulipa umaarufu sana ndani ya ccm

Monabani anatazamwa kama kada mwenye uchungu wa kuleta maendeleo ya harakaharaka ila siasa zake za kichungaji zinaweza zisihimili kishindo cha kumkabili mbunge wa sasa Godbless Lema ,hata hivyo amejizolea umaarufu sana kwa kusaidia jamii ikiwemo ujenzi makanisa bila kujali anapata nini.

Mrisho Gambo ni zao la UVCCM Mkoa wa Arusha,aliwahi kuwa mwajiriwa katika jiji la Arusha na baadaye alipata uteuzi wa kuwa Mkuu wa wilaya katika wilaya tofauti na baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha mwaka 2016 baada ya kufanikiwa kumng'oa kimizengwe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda (Kijiko)

Gambo ameonyesha wazi kutaka ubunge jimbo la Arusha akiwa na kumbukumbu ya machungu ya kutemwa ukuu wa Mkoa huku wapambe wake wakijinasibu kwamba hatua hiyo ni mbinu alizotengeneza ili kugombea ubunge na kuwa mbunge wa Arusha lakini siasa zake hazipewi kipaumbele na wanaccm kwa madai kwamba amejaa kiburi mwenye dharau asiyetaka kusikiliza ushauri wa watu wadogo akiwapa nafasi zaisi watu wenye pesa hasa wahindi.

Siasa za Gambo ni za kugawa wanachama kulingana na uwezo wao ila ni mchapakazi mzuri na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo katika jiji la la Arusha
Hususani Katika kata yake ya Muriet,Mfutiliaji na yupo makini na mtaalamu wa kutengeneza fitina.

Mwingine anayetajwa kugombea jimbo la Arusha mjini ni Lengai ole Sabaya Mkuu wa wilaya ya Hai,anayetajwa kama mwanasiasa kijana mwenye ushawishi na Msimamo usioyumbishwa ambaye ameonyesha wazi kuuchukia upinzani na kufanikiwa kumdhibiti mwenyekiti wa taifa wa chadema,Freemen Mbowe huku akiitetea serikali .

Mwaka 2015 wakati upinzani umepamba moto na wanaccm wengi kubaki nyuma ambapo yeye akiwa mwenyekiti wa uvccm,Mkoa alijipatia heshima katika kusimamia haki bila kuogopa wingi wa wafuasi wa chadema.

Baadaye Sabaya aliteuliwa kuwa DC wa hai na kujenga taswira ya ushawishi mwiongoni mwa wasaidizi wa rais wanaomwelewa rais anachohitaji,hata hivyo Sabaya anatajwa kama kijana mwenye maono na uwezo mkubwa wa kupambana na siasa za kibabe katika jimbo la Arusha ambapo wanaccm wamemshawishi agombee maana wanamini hakuna mwanasiasa mwingine mwenye uwezo wa kupambana na Lema.

Wengine ni Thomas Munis na Albert Msando hawa majina yao yanaumaarufu sana kwa nafasi zao ila wanaweza wa kwa cha huo kwa tu iwapo watazichanga vema karata zao vukizingatia kwamba Munisi ama Brigedia tiyari anamtaji wa kura za maoni baada ya mwaka 2015 kugombea na kupata kura za kutosha ndani ya ccm.