Baada ya wiki kadhaa za maandamano ya kupinga ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi nchini Marekani, Rais Donald Trump hapo jana amesema serikali yake itawekeza zaidi katika mafunzo ya polisi na kuchukua hatua za kuwajengea uwezo wa mitaji ya biashara ndogo ndogo kwa jamii ya wachache nchini humo.
Katika hafla moja ya kanisani mjini Dallas, Rais Trump amesema Marekani inahitaji jeshi madhubuti la polisi na haliwezi kupiga hatua kwa kuwaita mamilioni ya Wamarekani wabaguzi.
The post Trump: Marekani inahitaji polisi madhubuti appeared first on Bongo5.com.