Rais wa Marekani Donald Trump, amesaini amri ya kuifanyia mageuzi idara ya polisi nchini humo, mnamo wakati nchi hiyo inagubikwa na maandamano, kufuatia mauaji ya Wamarekani weusi mikononi mwa maafisa wa polisi.
Rais Trump amesema mageuzi hayo yanalenga kuleta haki. Amri hiyo ya Rais inatoa ufadhili kwa idara ya polisi kote nchini humo, na inapiga marufuku mbinu ya polisi kumkabili mshukiwa kwa njia inayomfanya asiweze kupumua kama hatua ya kumdhibiti, ila tu ikiwa maisha ya polisi yako hatarini.
Amri hiyo pia inahimiza mafunzo zaidi kuhusu miongozo ya kutumia nguvu, na pia ukusanyaji wa taarifa au data za polisi ambao wamejihusisha na mienendo mibaya.
Trump amesema wanapaswa kuachana na mbinu za zamani ambazo zimefeli, na kwamba kinachohitajika sasa si hofu na migawanyiko, bali kuimarisha uzingatifu wa sheria na kuzileta jamii pamoja.
The post Trump asaini amri ya mageuzi idara ya polisi appeared first on Bongo5.com.