Rais wa Marekani Donald Trump alijaribu kuomba msaada wa rais wa China Xi Jinping ili kushinda awamu ya pili ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka huu, mshauri wa zamani wa Trump wa Usalama wa Taifa John Bolton ameeleza katika kitabu chake kipya.

John Bolton claims Trump asked China for re-election help - CNN Video

Bolton ameandika hayo pamoja na madai mengine zaidi ya siri na ya kushangaza kumhusu Rais Trump, katika kitabu ambacho ikulu ya Marekani imeshitaki kutaka kisizinduliwe.

Game on': John Bolton's tell-all book reportedly taunts Trump ...

Bolton amedai kuwa nia ya Trump kutaka kuchaguliwa tena ndiyo imekuwa msingi wa sera yake ya mambo ya kigeni. Kitabu hicho kinachoitwa “The Room Where it Happened” yaani Chumba ambacho kilitokea’ kinatarajiwa kuzinduliwa Jumanne ijayo.

Bolton alikuwa mshauri wa Trump kuhusu masuala ya usalama wa kitaifa kwa muda wa miezi 17, kabla ya kujiuzulu.

The post Trump aliomba usaidizi kutoka China kushinda awamu ya pili ya Urais – Aliyekuwa Mshauri wa Trump aanika appeared first on Bongo5.com.