Kupitia EATV & EA Radio Digital, tunakupa historia ya kukurudisha miaka ya nyuma tangu ulipotoka wimbo wa nilikataa ya TID na Q Chief "Top Band", ambayo walimshirikisha Mr Blue.Kwenye  video ya wimbo huo yupo msanii wa filamu Irene Uwoya, na TID amesema kwa kipindi kile alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo huyo, japo hakutaka kutangaza ila kuna muda anatamani kurudiana naye.

"Kipindi kile Irene Uwoya ilikuwa ni kazi yangu, lakini si unajua tena kinyamwezi hadi kwenye video, nilikuwa nam-date alikuwa ni mpenzi wangu,  nilikuwa sio mtu wa kuonyesha kama natoka naye ilikuwa ni vitu binafsi, kipindi kile alikuwa wamoto kuna muda natamani ku-date naye tena" amesema TID.

Ishu nyingine kuhusiana na wimbo huo ni pale Q Chief, alipomfuata na Polisi kisha kumlipa Milioni 2 kutokana na madai na hakimiliki ya kazi waliyoifanya.