Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amevamiwa na watu watatu waliomkanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia.

Hayo ameyabainisha mapema leo Juni 9, 2020, na kusema kuwa taarifa kamili wataitoa hapo baadaye.

"Zipo taarifa kwamba Mh Mbowe amevamiwa na watu watatu, wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia, lakini tunafuatilia tutatoa taarifa kamili baadaye na yuko Hospitali ya Ntyuka wodi namba 4" amesema Kamanda Muroto.

Taarifa zinaarifu kuwa Mbowe ameshambuliwa majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia leo.