•√ Mkali wa HipHop Bongo Stamina, amefunguka na kusema suala la kuombana msamaha aliyekuwa mkewe  ni jambo la siri na  la watu wawili, kwani wakati wanakubaliana kuwa kwenye mahusiano hakuwaambia watu.

•√ "Mimi sijaweka mahusiano yangu wala kumuonyesha mke wangu, ule ni mziki tu halafu sijui kwanini Watanzania hawaamini kwamba naweza nikamuimbia mtu mwingine, nimeongelea ndoa sijamuongelea mwanamke wangu".

•√ "Masuala ya kuombana msamaha ni mambo binafsi ya watu wawili, kama yeye ameomba msamaha au mimi nimeomba msamaha ni vitu binafsi na hata ikitokea hivyo lazima ianze kwa watu wawili siwezi kuja kuvisema hadharani kwa watu".