NYUMA ya madai kwamba, mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amebeba ujauzito wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kuna siri nzito ambayo sasa imefichuka.

 

TUANZE NA MADAI YALIYOPOGhafla tu Mji wa Instagram umechafuka, kubwa ni madai mazito kwamba Poshy Queen ambaye pia ni mjasiriamali maarufu, amebeba mimba yenye umri wa miezi minne ambayo mhusika wake ni Diamond au Mondi.

 

Ishu hiyo imesimamisha ubuyu mwingine wowote kwenye kurasa za udaku pale Instagram, kwani inavyoonekana mashabiki wengi wanavutiwa na muunganiko (kapo) ya Poshy Queen na Mondi au Simba kutoka Tandale.

 

Mondi anafahamika kuwa ni staa mkubwa wa muziki barani Afrika, lakini pia Poshy Queen naye ni mrembo mwenye umbo matata kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), hivyo kuonekana kuwa ni kapo ya moto mno.Madai haya mazito ya Mondi kumpachika kibendi Poshy Queen, yanakuja miezi kadhaa baada ya Simba kuachana na mama mtoto wake mwingine, Tanasha Donna, raia wa nchini Kenya.

 

KABLA YA MADAI YA UJAUZITO
Hata hivyo, kabla ya madai ya Poshy Queen kumbebea Mondi ujauzito, kumekuwa na madai ya chinichini kuwa, wawili hao wanafanya kweli.Wapo watu wa karibu na wawili hao ambao wanadai kujua kila kitu juu ya uwepo wa ukaribu unaoacha maswali baina ya mastaa hao.

 

UKARIBU NA FAMILIA
Uchunguzi wa gazeti hili wa muda mrefu ulibaini kwamba, Poshy Queen ana ukaribu mkubwa mno na familia ya Mondi hasa mama wa staa huyo, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ na dada’ke, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.Chanzo cha karibu kilinyetisha kuwa, Poshy Queen amekuwa hakauki kwenye matukio mbalimbali yanayohusisha familia hiyo kiasi cha kudaiwa kumuweka mkononi Mama Dangote na Esma.

 

SIRI YA MONDI NA POSHY

Gazeti hili linafahamu kwamba, siri ya Mondi kuwa na ukaribu na Poshy Queen ilianzia pale kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

 

Mondi na Poshy Queen walikutana pale Mlimani City usiku ule wa Julai 7, 2019 katika tukio kubwa la kuadhimisha siku ya kuzaliwa (birthday) ya Mama Dangote na aliyekuwa mkwewe, Tanasha ambazo ziligongana.Usiku huo uliojaa vibweka vya mastaa wa Bongo, ulipewa jina la 707 GATSBY.

 

Huu ndiyo usiku ambao Mondi aliwazawadia wawili hao magari mapya ya kifahari, kila mmoja ambapo Mama Dangote aliondoka na Toyota Land Cruiser V8 huku Tanasha akijitwalia Toyoya Prado V8, yote yakiwa na gharama ya zaidi ya shilingi milioni 300 za Kibongo.

TWENDE UKUMBINI
Ndani ya ukumbi huo, ndipo Wasema Chochote (ma-MC) wa shughuli hiyo ambao ni wachekeshaji, Slyvester Mujuni ‘Mpoki’ na Eric Omond wakamuita mbele ya Poshy Queen ili afungue shampeini, lakini haikufahamika kama walifanya hivyo kwa maelekezo au utashi wao wenyewe.Lakini mbali na Poshy Queen, Mpoki pia alimuita mbele mwigizaji wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo’ ambapo kwa pamoja walifanya shughuli ya kufungua shampeini.Wakati wakifungua shampeni, Mpoki alisikika akisema; “Hii inaweza kuwa kapo mpya mjini!”Tukio hilo lilionekana kupandisha mizuka ya wengi, lakini waliotia fora walikuwa Mama Dangote na Esma.

 

KUCHEZA MUZIKIU
lipofika muda wa kucheza muziki, kila mtu alikuwa na mtuwe, Mama Dangote na Anko Shamte wake, Esma na Petit Man Wakuache, Mondi na Tanasha wake, lakini ikasemekana jamaa alikuwa akimkata jicho meneja wake, Sallam SK aliyekuwa anaserebuka na Poshy Queen.

 

Muda mfupi baadaye, watu walirejea kwenye viti vyao na hapo ndipo lilipojiri tukio ambalo linatajwa kuwa chanzo cha Mondi na Poshy Queen kuwasiliana na mengineyo.Nyuma ya Mondi na Tanasha kulikuwa na Esma, Sallam na Poshy Queen na pembeni yao kulikuwa na DJ wa Mondi, Rommy Jones na hapo ndipo Mondi alipogeuka na kudaiwa kubadilishana namba za simu na mrembo huyo mbele ya Tanasha.

MONDI ALIPATA WAPI UJASIRI?
Tukio hilo liliibua minong’ono mno huku kila aliyeliona akijiuliza; “Diamond amepata wapi ujasiri huu wa kuchukua namba ya demu mwingine mbele ya demu wake?”Hata hivyo, wakati tukio hilo likijiri, Tanasha alionekana waziwazi kutolifurahia, hivyo nuru ikampotea ghafla usoni na kuonekana kama amemaindi.

NDIVYO SINEMA ILIVYOKUWAHivyo ndivyo sinema ya Mondi na Poshy Queen ilivyoanza na sasa madai ni kwamba Mama Dangote anatarajia mjukuu wa nne kutoka kwa Poshy Queen baada ya Tiffah Dangote na Nillan kutoka kwa Zari, Dyllan kwa Hamisa Mobeto na Naseeb Junior kutoka kwa Tanasha.

HUYU HAPA POSHY QUEENI
li kumaliza ubishi kama kweli ana kibendi cha Simba, gazeti hili la RISASI JUMAMOSI lilimvaa Poshy Queen ambapo mambo yalikuwa hivi;

RISASI JUMAMOSI: Mambo vipi Poshy Queen?

POSHY QUEEN: Poa, nani mwenzangu?

RISASI JUMAMOSI: Unaongea na mwandishi wa Gazeti la RISASI, kuna hizi habari zinasambaa kwa kasi mitandaoni kwamba una ujauzito wa miezi minne wa Diamond, halafu mwenyewe ameukataa, je, ni kweli?

POSHY QUEEN: Hizo ni tetesi tu za watu. Watu wakiamua kusema wanasema wanachoweza. Mimi sijawahi kutembea na Diamond na wala sina huo muda wa kutembea na huyo mwanaume. Sina mimba yake kama inavyoongelewa huko mitandaoni.

RISASI JUMAMOSI: Ni kweli kwamba ulikuwa na mwanaume anayekuweka mjini, hivyo baada ya yeye kusikia kuwa umebeba mimba ya Mondi akakutelekeza na sasa umefulia hadi umefunga duka?

POSHY QUEEN: Sijafilisika wala sijafunga duka, nimelihamishia Kijitonyama (mwanzoni lilikuwa Sinza-Kamanyola jijini Dar) ila kwa sasa ipo kwenye matengenezo, hivyo tunauza vitu online (mtandaoni) mpaka ofisi itakapokuwa tayari, lakini kwa sasa wateja wangu wanapata huduma mtandaoni.

MAMA DANGOTE ANASEMAJE?Alipotafutwa Mama Dangote alisema; “Hakuna kitu kama hicho, hizo ni habari za mitandaoni.”

HITIMISHOMondi amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na warembo mbalimbali wa ndani ya nje ya Bongo huku wengine wakimtamani bila mafanikio.