Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea jana kwa mechi mbili zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Simba walishuka dimbani kwenye uwanja mkuu wa taifa kucheza na Maafande wa Ruvu Shooting, mchezo ambao uliisha kwa sare ya magoli moja kwa moja.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 12 kupitia Shiza Ramadhani 'Kichuya', goli ambalo lilidumu kwa dakika 24 pekee baada ya nahodha wa Ruvu Shooting Fully Zulu Maganga kusawazisha kunako dakika ya 36.

Kwa kupata alama moja kwenye mechi hiyo Simba wanaendelea kuwa vinara wa ligi ambapo wanfikisha alama 72 kwenye msimamo, huku Ruvu Shooting FC wakifikisha alama 40 katika nafasi ya 11 kwenye msimamo.