SIMBA wanautaka ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara baada ya nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco, kusema sasa wapo tayari kuendelea na mechi zilizobaki kumalizia kazi ya kubeba ubingwa.

Bocco ametoa kauli hiyo Simba ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 71 baada ya kucheza mechi 28. Imebakiwa na mechi kumi kumaliza msimu huu ambapo kati ya hizo, ikishinda tano tu inakuwa bingwa.

Bocco amesema: “Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mapambano ya kumalizia ligi, tunachosubiria ni kuingia uwanjani na kuanza kupigania ubingwa wetu katika sehemu ambayo imebaki.

Juni 14, Simba itakuwa na kete ya kwanza ya kumenyana na Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa baada ya ligi kusimama kutokana na janga la Virusi vya Corona.