Mkurugenzi wa kampuni ya uwakala wa wachezaji nchini @shaffihdauda_ amefafanua na kuweka wazi kuwa yeye sio Wakala wa wachezaji kama watu wengi wanavyohisi bali ana kampuni ya uwakala wa wachezaji ambayo imesajili na kutambuliwa na FIFA @shadakasports


Akiongea baada ya tukio fupi la birthday dinner ya mmoja wa mawakala wa wachezaji wanaofanya kazi chini ya kampuni hiyo IBRAH DIGALA ameeleza kuwa yeye hausiki kabisa na mambo ya uwakala bali yeye ana kitengo chake katika kampuni hiyo ingawa ina watu wengi mpaka hivi sasa.

Kampuni ya @shadakasports imekuwa ikihusika kuwatoa wachezaji wa Kitanzania nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuendeleza carrier zao za soka kupitia kwa wakala aliyopo chini ya @shadakasports bwana IBRAH DIGALA.

The post Shaffih dauda: Mimi sio wakala wa wachezaji bali nina kampuni pia nina Connection (+Video) appeared first on Bongo5.com.