Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amevamiwa na watu watatu waliomkanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia.

Hayo ameyabainisha mapema leo Juni 9, 2020, wakati akizunggumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kusema kuwa taarifa kamili wataitoa hapo baadaye.

“Zipo taarifa kwamba Mh Mbowe amevamiwa na watu watatu, wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wake wa kulia, lakini tunafuatilia tutatoa taarifa kamili baadaye na yuko Hospitali ya Ntyuka wodi namba 4” amesema Kamanda Muroto.

Imeelezwa kuwa Mbowe ameshambuliwa majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia leo.

https://bit.ly/2UpeRXQ

The post RPC Dodoma Muruto, aelezea jinsi Mbowe alivyokanyangwa kanyagwa na watu watatu – Audio appeared first on Bongo5.com.