Mwigizaji na mwimbaji @rotimi amekamata namba 1 kwenye orodha ya nyimbo 50 zilizotafutwa zaidi (The Most Shazamed tracks) kwa siku 7 katika Jiji la New York kwenye mtandao wa Apple Music, kupitia wimbo wake "In My Bed" aliompa shavu Wale.

Rotimi ambaye ni mpenzi wa mwimbaji Mtanzania Vanessa Mdee, amekaa juu ya wakali wa dunia kama Chris Brown, Young Thug na Lil Baby.