Rapa kanye west azidi kuishangaza dunia kutoka kwenye deni la USD 53MILLION Mpaka kuwa Rapa Tajiri zaidi duniani akiwa na thamani ya USD 1Billion na sasa fobres wamedondosha orodha mpya ya wasanii waliotengeneza mkwanja mrefu 2020,Kanye west Toka ($150 million) mwaka 2019 hadi ($170 million) mwaka 2020, Kanye West ametajwa kuongoza orodha ya Forbes kwa wanamuziki waliolipwa/tengeneza pesa nyingi zaidi katika kipindi cha mwaka mzima kuanzia Juni 2019 hadi Juni 2020.

Orodha hiyo mpya iliyotolewa leo imemuweka Kanye kwenye nafasi ya kwanza, akitengeneza kiasi cha bilioni 393.8 za Kitanzania kabla ya kukatwa kodi na ni katika kipindi cha miezi 12, fedha ambazo kwa asilimia kubwa zimetajwa kutokana na kampuni ya Yeezy.

Nafasi ya pili imeenda kwa mwanamuziki nguli wa Uingereza Elton John, huku Top 5 ikikamilishwa na Ariana Grande, Jonas Brothers (Nick Jonas, Joe Jonas, Kevin Jonas) na The Chainsmokers.

Taylor Swift ambaye aliongoza orodha ya mwaka 2019, ametupwa nafasi ya 7. Jay-Z yupo nafasi ya 12, Drake 15, na Rihanna 18.

HII HAPA TOP 10

World's Highest Paid Musicians of 2020
(Forbes)
-
1. Kanye $170M
2. Elton John $81M
3. Ariana Grande $72M
4. Jonas Brothers $68.5M
5. Chainsmokers $68M
6. Ed Sheeran $64M
7. Taylor Swift $60M
8. Post Malone $59M
9. Rolling Stones $59M
10. Marshmello 56M