Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ya CCM Makao Makuu ya Mkoa Dodoma mara baada ya kupata wadhamini wa Chama chake cha Mapinduzi CCM. PICHA NA IKULU

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Juni, 2020 amechukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.


Rais Magufuli amechukua fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, na amekabidhiwa fomu hizo na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa aliyekuwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndg. Rodrick Mpogolo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Uchumi na Fedha Dkt. Frank Haule.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hizo na kulipia ada ya shilingi Milioni 1, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru CCM kwa kumpa fomu hizo na amewaomba wana CCM na Watanzania wote wamuombee katika safari yake ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha Urais.


Mhe. Rais Magufuli amewaomba wana CCM wamdhamini na washiriki katika mchakato wa uchaguzi kwa amani, utulivu na mshikamano.


Baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameanza safari ya kutafuta wadhamini ambapo amekwenda Ofisi ya CCM Mkoa wa Dodoma na kumkabidhi fomu ya wadhamini 25 Katibu wa Mkoa Bi. Jamila Yusuph.


Mhe. Rais Magufuli amekutana na wanachama wachache wa CCM waliokuwa katika Ofisi ya Makao Makuu na Ofisi ya Mkoa ambapo amewatakia heri katika mchakato wa uchaguzi unaoendelea na amewataka kuendelea kukiimarisha chama.Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

17 Juni, 2020