Kiasi cha watu 107 wamekufa baada ya kupigwa na radi kwenye maeneo ya Kaskazini na Mashariki ya India wakati taifa hilo likijitayarisha na msimu wa mvua kubwa za masika ambazo kila mwaka husababisha maafa makubwa.

India: More Than 100 People Killed By Lightning Strikes | News ...

Maafisa nchini India wamesema takriban watu 83 wamepoteza maisha katika jimbo masikini la Bihar baada ya kukumbwa na miale ya radi huku wengine 24 wamekufa katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh.

Lightning strikes kill at least 107 in India

Mkuu wa idara ya kuzuia majanga wa jimbo la Bihar amesema hiyo ni moja ya idadi kubwa kabisa ya vifo vilivyotokana na radi kuwahi kurekodi ndani ya siku moja kwenye jimbo hilo katika miaka ya karibuni.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kuongeza kuwa serikali za majimbo zinachukua hatua ya kutoa msaada unaohitajika.

Imeandikwa na Hamza Fumo

The post Radi yaua zaidi ya watu 100, India appeared first on Bongo5.com.