Derek Chauvin, polisi wa zamani ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya George Floyd, amewekewa dhamana ya dola za Kimarekani milioni 1.25

Derek Chauvin taken into custody after George Floyd death | Daily ...

Chauvin mwenye umri wa miaka 44, aliunganishwa na kikao cha mahakama kwa njia ya video akiwa gerezani, mjini Minneapolis, jimbo la Minnesota.

Jaji anayeendesha kesi hiyo alitangaza masharti kadhaa ya kuwachiwa kwake kwa dhamana. Mshukiwa huyo hapaswi kuondoka jimbo la Minnesota baada ya kuwachiwa, asiwasiliane na familia ya Floyd na lazima asalimishe silaha zote anazomiliki.

Bail raised to $1.25 mln for Derek Chauvin in Floyd death case - CGTN

Aidha haruhusiwi kufanya kazi katika nafasi yoyote kwenye idara ya usalama. Polisi wengine watatu wa Minneapolis walifikishwa mahakamani wiki iliyopita wakikabiliwa na mashitaka ya kusaidia katika mauaji ya Floyd. Wote wanne wamefutwa kazi.

The post Polisi mshukiwa wa mauaji ya Floyd aachiwa kwa dhamana ya dola milioni moja appeared first on Bongo5.com.