Polisi nchini Nigeria wamemkamata mtu wanayedai kuwa amewabaka wanawake 40 katika mji mmoja katika kipindi cha mwaka mmoja .

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Abdullahi Haruna, mtu huyo alikamatwa baada ya mwanamke mmoja katika mji wa Dangora kaskazini mwa Nigeria kumpata akiwa amejificha katika chumba cha watoto kulala. Bw. Haruna aliongeza kuwa mtu huyo alijaribu kutoroka lakini majirani walimkimbiza na kumshika.

Kumeshuhudiwa msururu wa ubakaji na mauaji ya wanawake katika siku za hivi karibuni Nigeria, hali ambayo imesababisha hasira miongoni mwa wananchi, huku maelfu yao wakitia saini ombi la kupinga uovu huo na kutaka hatua zichukuliwe kwa kutumia hashtag #WeAreTired.

Dangora ni mji mdogo katika jimbo la Kano karibu kilomita 85 kusini -magharibi mwa jimbo hilo, hali ambayo inawafanya polisi kutofika kwa muda unaostahili, anasema mwandishi wa BBC Mansur Abubakar kutoka Kano.

Map of Nigeria

Chifu kiongozi wa mji huo, Ahmadu Yau, alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua muhimu kuelekea kukabiliana na uhalifu huo.

“Watu wa Dangora wanafurahia sana hatua zilizochukuliwa na tunatumaihaki ya itatekelezwa.”

Wakaazi walisema kwamba mwaka jana waliishi kwa uwoga,hata ndani ya nyumba zao, kwa sababu walidokezewa wabakaji wanaruka ua na kuingia majumbani kuwabaka wanawake.

“Sasa tunaweza kufunga macho na kulala kwa amani,” mmoja wa wanawake aliongea.

Presentational grey line

Hali ni mbaya kiasi gani Nigeria

  • Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uwavera Omozuwa alidaiwa kufariki baada ya kubakwa ndani ya kanisa na baadaye kugongwa kichwani kwa kutumia kifaa butu, mshukiwa amekamatwa.
  • Msichana wa miaka 12- alinajisiwa miezi miwili iliyopita kaskazini – magharibi mwa jimbo la Jigawa; watu 11 wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho.
  • Tina Ezekwe aliuawa na polisi kusini-magharibi mwa jimbo la Lagos; polisi wawili wamekamatwa
  • Barakat Bello alidaiwa kuwabakwa na genge la wanaume na kuuawa kusini -magharibi mwa jimbo la Oyo; hakuna hata mshukiwa mmoja aliyekamatwa.
  • Msichana wa miaka 17-alibakwa na genge la wanaume kusini -magharibi mwa jimbo Ekiti; watu wawili wamekamatwa.

The post NIGERIA: Akamatwa na Polisi kwa kubaka wanawake 40 appeared first on Bongo5.com.