Mkali wa Album ya "Afro East" Harmonize, amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, kuhusu muonekano na style yake ya nywele ya kusuka ambayo ilikaa kwa muda mrefu kichwani kwake, kisha kuitoa na kusema anatamani kuirudia."Ile style nilijaribu kufanya kitu cha tofauti, nasikitika nilizitoa kwa sababu ya mwezi wa Ramadhan na mimi ni muislam nafunga nikaona nizitoe, nilikuwa nazipenda na natamani nirudi kwenye style ile kwa sababu, inanifanya nionekane wa tofauti na mtu akiniangalia anaiona ni msanii mwerevu kutoka Afrika Mashariki na najivunia hilo" amesema Harmonize.

Akizungumzia kuhusu dini yake na kuishi kwenye style ya kusuka, kuvaa hereni na kuchora tattoo Harmonize amesema
 "Kila unachokifanya kwenye maisha tambua kwamba Mungu anakupa muongozo hata kipaji nilichonacho yeye ndiyo amenipa, siwezi kujutia kufanya vitu ambavyo vitanifanya nionekane kama msanii kama  kusuka nywele, kuchora tattoo au kuvaa hereni kwa kuwa namuheshimu na nikipata nafasi nasali".