Drake amechangia kiasi cha ($100K) sawa na TSH. 200M kwa ajili ya kuwawekea dhamana Waandamanaji ambao wanashikiliwa na polisi katika maandamano ya kupinga ukatili wa polisi na kuhitaji haki itendeke kufuatia mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd.

Hamasa ya Drake kuchangia kiasi hicho imekuja baada ya mshairi maarufu na mwimbaji wa mjini Toronto Mustafa kuchangia ($400) na kisha kumtaka Drizzy afanye hivyo. Baadaye Drake alijiongeza na kuweka risiti ya mamilioni kwenye insta story yake.