Mwanaume anaeitwa Simon Louis (49) amekataliwa ombi lake na mpenzi wake la kumuoa Mary Emmanuella (41) ambaye ni mpenzi wake aliyempenda mpaka kuokoa maisha yake mara baada ya kujitolea figo yake kumpandikizia na kunusuru maisha yake pindi figo zake zilipofeli.

Hata hivyo Simon alipohojiwa na Mwandishi wa Metro UK alisema kuwa hajutii maamuzi yake ya kumpa figo mwanamke huyo aliyempenda hata mara baada ya kukataa ombi lake alipopona ugonjwa uliokuwa unamsumbua.

“Nilimpa moyo wangu, lakini pia nilijifikiria nikampa na figo yangu, chochote kilichotokea sijutii wala sitojutia kwa kumpa zawadi ya maisha,” amesema Simon.

Aidha Mary Emmanuella amesema ataendelea kuwa rafiki wa karibu wa Simon.

“Ni rafiki yangu sana na daima itakuwa hivyo, mapenzi kati yetu ni ya kweli, Simon angefariki kwa kile alichokifanya kwa ajili yangu,” amesema Simon