Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook imeondosha mtandaoni matangazo ya kampeni ya rais Donald Trump kwa kutumia alama zilizokuwa za utawala wa kinazi wa Ujerumani.

Facebook imesema tangazo lililolengwa lilikuwa na alama ya pembe tatu nyekundu kama iliyotumika na utawala wa kinazi kuwatambua wapinzani wao kama wakomunisti.

Matangazo hayo ni sehemu ya kampeni ya Trump kwa uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Timu ya kampeni ya Trump imesema kuwa tangazo hilo lilikuwa linakilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto antifa, ambacho wanadai kinatumia nembo hiyo.

Facebook inadai matangazo hayo yanaenda kinyume na sera yake ya chuki ya kupangwa.

“Haturuhusu alama ambazo zina simama kwa mirengo ama makundi ya chuki, labda iwe ni kukemea jambo hilo,” imeeleza Facebook.

A screenshot showing a Trump campaign ad that was removed from Facebook, 18 June 2020Picha iliyopigwa kuchukua alama zilizotumiwa na kampeni ya Trump na kuondolewa kutoka mtandao wa Facebook

“Hiko ndicho tulichokiona kwenye tangazo hili, na popote pale alama hiyo itakapotumika tutachukua hatua kama hii,” ameeleza mkuu wa sera za ulinzi wa Facebook Nathaniel Gleicher.

Matangazo hayo, ambayo yalipakiwa kwenye kurasa za mtandao wa Facebook za Trump na Makamu wake Mike Pence yalifutwa baada ya kuwa mtandaoni kwa saa 24.

“Pembe tatu nyekundu ni alama inayotumiwa na antifa, hivyo ilitumika katika tangazo kuhusu antifa,” ameeleza Tim Murtaugh, msemaji wa timu ya kampeni ya Trump.

“Pia tnatambua kama Facebook wana kibonzo (emoji) cha pembe tatu nyekundu pia ambacho ni sawa kabisa tuliytumia,” ameongeza.

Trump katika siku za hivi karibuni amelishutumu kundi la antifa kwa kuanzisha maandamano ya vurugu kote nchini Marekani kufua kifo cha mtu mweusi George Floyd mikononi mwa polisi.

Rais Trump alitishia mwezi uliopita kuwa atalitangaza kundi hilo linalopingana na itikadi za kifashisti kuwa “kundi la kigaidi la ndani ya nchi”, ijapokuwa wataalamu wa sheria hawana hakika kama ana uhalali wa kufanya hivyo.

Antifa ni kundi la maandamano la mrengo mkali wa kushoto ambalo linapingana na unazi, ufashisti, ukimya wa weupe na ubaguzi wa rangi.

Linatajwa kuwa ni kundi lisilo na uongozi maalumu, na waandamanaji wake wanapinga sera za Trump dhidi ya uhamiaji, utaifa na Waislamu.

The post Mtandao wa Facebook wafuta maatangazo ya kampeni ya Trump, Sababu zaelezwa appeared first on Bongo5.com.