MBUNGE wa Iringa mjini (CHADEMA) Peter Msigwa, leo Juni 14, 2020 ametangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020.

Alichokisema Peter Msigwa

“Leo natangaza rasmi ni yangu ya kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tayari kwa mujibu wa taratibu na katiba ya CHADEMA nimeshawasilisha taarifa rasmi ya kuomba kuteuliwa na chama kugombea Urais wa JMT

”Nimesukumwa na jambo moja la msingi kutaka kuwania nafasi hii ya juu kabisa. Nataka kuongoza mageuzi makubwa ya kiutawala,kiuchumi,kielimu, yatakayoleta maendeleo makubwa na ya haraka. Yaliyo jumuishi na endelevu kwa manufaa ya sasa na Tanzania ijayo”