Msanii wa HipHop Bongo Wakazi ametia nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Segerea kupitia chama cha ACT Wazalendo kwenye uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakazi (kushoto) akikabidhiwa kadi na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe.

Wakazi ameeleza nia hiyo leo Juni 20, 2020 kwenye mkutano wa chama hicho unaofanyika jijini Dar es salaam.

Wakazi amesema amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu wa masuala ya haki na usawa hivyo ameona ni wakati sasa wa kuwa kiongozi.

”Kwasababu nimepata heshima ya kuitwa hapa mbele ya mkutano naomba nitumie nafasi hii kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika Jimbo langu la Segerea”, amesema.

Hivi karibuni Wakazi alikabidhiwa kadi ya chama hicho na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe.

Chanzo Eatv.tv

The post Msanii Wakazi ajitosa kwenye Ubunge rasmi, ataja jimbo atakalogombea appeared first on Bongo5.com.