Msaidizi mkuu wa Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na kazi ngumu kutokana na hatia ya ufisadi.

Kotu ta daure Vital Kamerhe a Kwango | Labarai | DW | 11.06.2020

Vital Kamerhe, mwenye umri wa miaka 61 na aliyehudumu kama mkuu wa utumishi kwenye Ikulu ya Kinshasa, alitiwa hatiani kwa ufisadi wa zaidi ya dola milioni 50, kwa mujibu wa Mahakama Kuu mjini Kinshasa.

Sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 1,500 chini ya programu iliyotangazwa na Tshisekedi mara tu baada ya kuapishwa Januari 2019.

Hii ni mara ya kwanza kwa wale wanaochukuliwa kama vigogo wasiogusika nchini Kongo kushitakiwa na kuhukumiwa kwa ufisadi. Kamerhe, ambaye anatambulika kama mwanasiasa mjanja anayecheza karata zake takribani katika kila utawala, alikuwa pia mshirika mkuu wa rais wa zamani, Joseph Kabila, kabla hajaungana na kambi ya Tshisekedi.

Hatoruhusiwa kuwania wadhfa wowote kwa miaka 10 baada ya kuhudumia hukumu yake na hata kushikilia wadhfa wowote wa serikali. Kamerhe amekana kuiba fedha zilizotengewa mradi wa ujenzi wa nyumba za serikali chini ya uogozi wa rais Tshisekedi na kuyataja mashtaka hayo kuwa ya kisiasa. Wakili wake Jean Marie Kabengela Ilunga aliutaja uamuzi huo kama ukiukaji wa haki za kibinadamu na kusema kwamba atakata rufaa.

The post Msaidizi mkuu wa Rais wa DRC afungwa miaka 20 jela appeared first on Bongo5.com.