Aliyekuwa naibu rais wa Marekani Joe Biden atakayewania urais dhidi ya Trump katika uchaguzi wa mwezi Novemba, ameapa kukabiliana na ubaguzi na kupigania marekebisho katika idara ya polisi kufuatia mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd mikononi mwa polisi.

Katika maoni yaliochapishwa katika gazeti la Los Angeles siku ya Jumamosi, Biden alizungumzia kuhusu haja ya kubuniwa kwa ”Sera mwafaka ambazo zinapaswa kuwa tayari zimebuniwa na kurekebisha hali ya ubaguzi,”

Biden aliongeza kusema kuwa sera za kijamii zinapaswa kutekelezwa na kuhakikisha kuwa kila idara ya polisi nchini humo inafanya tathmini kamili ya ajira ya maafisa wake na mafunzo yao huku serikali ya shirikisho ikitoa vifaa na rasilimali zinazohitajika kufanya marekebisho.

The post Mpinzani wa Trump uchaguzi ujao wa urais aahidi marekebisho idara ya Polisi  appeared first on Bongo5.com.