Mamlaka nchini china zimetoa taarifa za kufunga maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi kufuatia mlipuko mpya wa virus vya corona ambapo watu kadhaa wamepimwa na kubainika kuwa na corona.

Askari waliovalia sare za kuonesha nchi imerejea kwenye vita dhidi ya adui corona wameonekana wakipita kwa doria la vikundi ili kuwataka wananchi kujifungia.

Msemaji wa Serikali ya jiji la Beijing amewaambia watu kuwa kuna idadi kubwa ya watu waliobainika wana corona na kufunga maduka makubwa na maeneo ya mikusanyiko

Serikali ya China inanuia kuchukua hatua zaidi ndani ya saa 24 kudhibiti tukio la mlipuko huu mpya wa ugonjwa wa Corona.

The post Mlipuko wa corona China warudi tena, Beijing yawekwa lockdown appeared first on Bongo5.com.