Staa wa muziki kutoka New Jersey nchini Marekani mwenye asili ya Senegal Aliaume Damala Badara Akon Thiam alimaarufu Akon, amepokea kiasi cha Tsh Trilioni 13 kutoka kwa kampuni ya uhandisi nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Akon City nchini kwao Senegal.
Msanii wa nchi ya Senegali anayefanya shughuli za kimuziki nchini Marekani
Akon aliingia mkataba wa ujenzi huo mnamo Juni 6, 2020 na alipokea pesa hizo kutoka kwa wawekezaji ambao wanataka kukuza maendeleo ya mji huo, katika awamu mbili za ujenzi.
Katika hatua ya kwanza ya ujenzi huo unatarajiwa kumalizika mwaka 2023, huku vitu vinavyotakiwa kujengwa ni Makazi, Barabara, Hospitali, Shule, Vituo vya polisi, Hoteli, Maduka makubwa, Kituo cha taka na Umeme wa jua.
Ujenzi wa awamu ya pili utaanza mwaka 2024 hadi 2029, kutajengwa na kutengenezwa vitu kama viwanja, hifadhi, vyuo vikuu, shule kubwa, hoteli, na sehemu ya soko kubwa la biashara.
Akon ni msanii anayefanya shughuli za kimuziki nchini Marekani ila kwao ni Senegal, na aliingia makubaliano mwezi Januari 2018 na Serikali ya nchini kwao, kuhusu maendeleo ya kujenga mji wake wa Akon City.
The post Mji wa Akon kugharimu tril 13, muonekano wa mji huo umekuwa kivutio appeared first on Bongo5.com.